Watalii sita wasombwa na maji Hells Gate ‘Lango la jehanamu’

Hell's Gate is named after a narrow break in its cliffs

Shirika la wanyamapori la Kenya KWS, limefunga hifadhi ya kitaifa ya Hell’s Gate kufuatia mafuriko yaliosababisha vifo vya watu wanne siku Jumapili.

Waliosombwa na mafuriko ni watalii sita raia wa Kenya na mtu mmoja raia wa kigeni.

Shughuli za kuwatafuta watu hao zimekuwa zikiendelea usiku kucha na tayari miili mingine miwili imeopolewa kutoka kwa maji.

Vyombo vya habari nchini Kenya vianripoto kuwa manusra waliwafahamisha maafisa wa hifadhi hiyo kuhusu tukio hilo ndipo shughuli za kuwatafuta wahasiriwa zikaanzishwa mara moja.

Afisa wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la Habari la AFP kuwa watu waliosombwa na mafuriko hayo na ambao hawajapatikana huenda ”wamefariki” kutokana na ushahidi uliotolewa na wale walionusurika mkasa huo.

Hell's Gate National Park

Hifadhi ya Hell’s Gate, limepewa jina hilo kutokana na vyanzo vyembamba vya maji yanayopita kati kati ya milima na ambayo husababisha mafuriko.

Eneo hilo linasifika kwa mandhari yake ya kupendeza ambayo pia imeangaziwa katika filamu ya The Lion King.

Hifadhi ya hiyo iliyobuniwa mwka 1984, pia ina vituo vitatu vya kukuza kawi ya mvuke.

chanzo: bbc swahili/ AFP

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.