Robert Mugabe afariki dunia

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95 nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Mugabe ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong’olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.

“Kamarada Mugabe alikuwa ni mwanga wa mapinduzi, mwana umajui wa Afrika ambaye aliyatoa maisha yake katika ukombozi na kuwawezesha watu wake. Mchango wake kwa taifa letu na bara (la Afrika) hautasahaulika…” ameandika Mnangagwa.

Mugabe alitupwa jela kwa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kuukosoa uongozi wa Rhodesia mwaka 1964.

Mwaka 1973, yungali gerezani alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Zimbabwe African Union (Zanu), ambacho alikuwa ni mwanachama mwanzilishi.

Baada ya kuachiwa kutoka gerezani, alikimbilia Msumbiji na kuongoza mapambano ya kijeshi ya kudai uhuru.

Licha ya kuwa mpiganaji wa vita vya kushtukiza, alisifika kwa kuwa mzuri kwenye majadiliano.

Mwaka 1980 akafanikiwa kuingia madarakani baada ya uchaguzi uliomaliza utawala wa walowezi wachache wa kizungu.

chanzo: BBC swahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.