ZEC yatangaza vituo vya uandikishaji

ZEC imewataka wale wanaokwenda kujiandikisha kuhakikisha kuwa wana vitambulisho vyao vya Mzanzibari Mkaazi na wale wanaohakiki taarifa zao wawe na vitambulisho vya kura na vya Mzanzibari Mkaazi kwa pamoja.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza vituo vya uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu yakiwa maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Continue reading “ZEC yatangaza vituo vya uandikishaji”

Jussa amvaa Zitto uongozi ACT

Jussa anakuwa mwanachama wa tatu wa ACT Wazalendo kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo, akitanguliwa na kiongozi anayetetea nafasi yake, Zitto Kabwe, na Joseph Mona, ambaye hivi sasa ni Katibu wa mkoa wa Katavi.

Mwanasiasa wa siku nyingi visiwani Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, amechukuwa fomu kuwania uongozi wa juu kabisa wa chama cha ACT-Wazalendo, chama ambacho alijiunga nacho mwaka jana baada ya kukihama chama alichoshiriki kukiasisi cha CUF, kufuatia mgogoro wa kiuongozi kati ya kambi ya Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba na ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. Continue reading “Jussa amvaa Zitto uongozi ACT”

Sasa ni rasmi, Maalim Seif kugombea

Makamu huyo wa kwanza mstaafu wa Rais wa Zanzibar anaingia kwenye kinyangànyiro ya uwenyekiti wa chama chake kipya ambacho alijiunga nacho mwaka mmoja uliopita.

Mshauri Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amerejesha rasmi fomu yake ya kuwania uwenyekiti wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwezi huu wa Februari 2020. Continue reading “Sasa ni rasmi, Maalim Seif kugombea”