Tag Archives: Tanzania

Taswira ya Upotoshaji Kwenye Mahusiano ya Waafrika na Waarabu

Waafrika na Waarabu: “Sisi Wazuri, nyinyi Waovu” au “Sisi Wazuri, na nyinyi Wazuri?”

Wengi tumeshuhudia katika mitandao tarehe 16 Oktoba, 2019, vinyago vya kustaajabisha sana kwa mtu yoyote ambaye anao uwezo wa kutumia akili yake vizuri. Tumeona ya mtu mmoja kavaa mavazi ya Kiarabu/Kiomani na kumchukua mtu aliyevaa winda na minyororo kama mtumwa wake na huku wakipita sehemu za Kariakoo, Dar es Salaam, wakitangaza kuwa asiyejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa atakuwa kama mtumwa wa Waarabu/Womani! Kwani atakuwa hana uwezo wa kuchagua viongozi wake. Kuyakoroga hayo mawili ni kufilisika kwa akili. Read more

Mabadiliko ya tabianchi yawakutanisha wataalamu wa Afrika

Mkutano wa kimataifa wa 53 wa utoaji wa utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za vuli katika nchi za Pembe ya Afrika pamoja na athari za tabianchi umefanyika Tanzania na kuwajumuisha wataalamu wa masuala hayo kutoka 11 za Afrika na mashirika ya kimataifa.

Akifungua mkutano huo wa siku tatu, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania, Isaac Kamwele, alisema ushirikishwaji wa watumiaji wa wataarifa za hali ya hewa ambao ni wananchi wa kawaida wakiwemo wakulima, wavuvi na wengineo ni muhimu sana katika kuepukana na majanga yanayojitokeza.

Alisema kuwepo kwa taarifa za mapema za utabiri wa hali ya hewa kwa wananchi, ni muhimu katika maandalizi ya kilimo pamoja na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na majanga kwa binaadam na mali.

Alisema alisema uchumi wa nchi zinazoendelea kama Tanzania zinategemea sana hali ya hewa ikiwa ni utalii, uvuvi na kilimo kwa hivyo taarifa za kitaalamu ni muhimu kuweza kuwafikia walengwa.

“Taarifa na tahadhari za mapema za hali ya hewa kama huu utabiri wa msimu ambao mtautoa hapa ni muhimu sana katika kufikia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi katika nchi zetu na ukanda wote wa Pembe ya Afrika” alisema Waziri  Kamwele.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Agnes Kijazi amesema serikali imekuwa ikitatua changamoto zinazoibabili mamkala hiyo ikiwa pamoja na kukunuwa vitendea kazi vya utabiri ili kutoa taarifa zinazotakiwa.

Alisema kwamba hivi sasa mamlaka imeweka rada mbili na imo katika mpango wa kuwema rada ya tatu kabla kutimiza rada saba zinazotakiwa kwa Tanzania nzima ikiwemo Zanzibar.

Mwakilishi kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dk Ernest Afiesimama  amesema kuwa bado zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitajika kushughulikiwa kwa pamoja ila kuleta ufanisi katika utabiri wa hali hewa kwa manufaa ya wananchi, hasa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, na ukame.

Naye Dk Guleid Artan, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha utabiri wa hali ya hewa Pembe ya Afrika (IGAD) amesema wamekuwa wakifanya kazi nzuri kuhabarisha wananchi kwa kutumia teknolojia za kisasa za utabiri wa hali ya hewa lakini mashirikiano miongoni mwa wadau yanahitajika zaidi.

Mratibu wa mkutano huo kutoka nchini Uganda bwana Patrick Luganda amesema kuna umuhimu wa watalaamu kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kujitayarisha na mabadiliko ya hali ya hewa kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo.

Mkutano huo unafanyika wakati ambao baadhi ya nchi za kiafrika khasa eneo la pembe hizo zikikabiliwa na ukame uliosababisha ukosefu wa mvua na kupelekea nchi hizo kushindwa kuendeleza kilimo na kukosekana kwa maji na chakula.

Nchi zinazoshiriki ni Kenya, Uganda, Somali, Ethiopia, Sudan ya kusini, Burundi, Rwanda, DJibouti na Eritrea na mwenyeji Tanzania ambazo kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa mvua utabiri wa kanda hutumika kuandaa wananchi kutokana na hali ya hewa itakavyokuwa kwa kutumia utaalamu wa kisayansi.

Mkutano huo umejumuisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka taasisi za hali ya hewa za Pembe ya Afrika, Taasisi za utafiti, Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Mashirika ya Kijamii, Wadau wa Maendeleo na Watoa maamuzi wa huduma za hali ya hewa katika sekta zote zinazotegemea sana huduma hizi za hali ya hewa.

Lengo la mkutano huo ni kujadiliana na kufikia mwafaka juu ya utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za vuli (Octoba hadi Disemba 2019) kwa nchi za ukanda wa Pembe ya Afrika.

Pamoja na hilo wataalamu hao watajadiliana namna ya kuandaa mikakati ya kukabiliana na hali mbaya ya hewa kwa msimu huo kwa kulenga sekta muhimu za kijamii na kiuchumi ambazo ni afya, kilimo, nishati, maji, usalama wa chakula, majanga, vita, vitisho na ukosefu wa amani katika nchi na kadhalika.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni utoaji wa tahadhari kwa hatua za haraka katika kukabiliana na athari za hali mbaya ya hewa “Early warning for Early Action in Support of Climate Resilience”.

Mkutano kama huo hufanyika kila mwaka katika misimu ili kutoa utabiri wa hali ya hewa na kuwasaidia wakulima na wananchi kwa ujumla katika kuchukua tahadhari zinazotokana na majanga na mabadiliko ya tabia nchi.

« Older Entries